Idara ya Afya

IDARA YA AFYA

Majukumu ya Idara ya Afya

1. Kutoa huduma za afya kwa wateja na wagonjwa kwa kufuata

sera na miongozo ya Wizara ya Afya.

2. Kuandaa mipango inayotilia mkazo mahitaji yote ya afya katika

Manispaa kwa kuzingatia miongozo kitaifa ya Afya

3. Kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinapatikana kwa wakati katika

vituo vya kutolea huduma za afya

4. Kukabiliana na magonjwa ya milipuko, maafa na kupanga

mipango ya kudhibiti na kuzuia.

5. Kutambua maeneo ya vipaumbele, kusimamia na kufanya utafiti

wa utendahji kazi katika Halmashauri.

6. Kuandaa na kuchambua taarifa za utekelezaji za afya katika

maeneo yote ya Afya

7. Kusimamia mikutano ihusuyo afya na kuratibu wadau wote

wanaosaidia huduma za afya katika Halmashauri

8. Kushirikisja jamii katika utoaji wa huduma za afya ili ishiriki

kikamilifu katika utoaji na usimamizi wa huduma za afya

9. Kusimamia utoaji wa huduma za afya katika maeneo ambayo

hayafikiki kirahisi ili kuhakikisha klinic tembezi inafanya kazi

10. Kufuatilia na kuthamini utekelezaji wa shunguli za afya kwenye

Halmashauri

11. Kutoa Elimu ya Afya kwa jamii juu ya kujikinga na magonjwa

mbalimbali.