Idara ya Elimu Msingi

IDARA YA ELIMU (MSINGI)

Majukumu ya Elimu (Msingi)

Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu katika mfumo rasmi na

Elimu nje ya mfumo rasmi katika manispaa. Aidha ni pamoja na

kuandaa.

1. Kuandikisha watoto wa darasa la kwanza wenye umri wa miaka

wa kwenda shule.

2. Kuelimisha jamii kushiriki katika mambo mbali mbali ya shule

kupitia vikao vya mitaa ambavyo wananchi watahudhuria na

kutoa maoni.

3. Kuandaa bajeti ya idara na vitengo vyake ikiwa ni pamoja na

mpango kazi unaoendana na bajeti hiyo.

4. Kusimamia na kuendeleza taaluma katika manispaa ya musoma

kwa kusimamia ufundishaji, ujifunzaji mahudhurio ya walimu,

wanafunzi na utendaji kazi kwa ujumla.

5. Kuandaa takwimu mbalimbali za kielimu za wanafunzi, walimu,

samani na miundombinu.

6. Kuratibu mashindano ya ya taaluma na michezo kwa shule za

msingi.

7. Kusimamia haki na maslahi ya walimu kwa kufuata taratibu

kama vile ruhusa, likizo masomo, matibabu n.k.

8. Kuhudumia jamii kuhusiana na mambo yote ya kielimu na

mafunzo mbalimbali kupitia kamati za shule na shuguli

nyinginezo kama vile uhamisho wa wanafunzi.

9. Kuandaa na kuendesha vikao mbalimbali vya wadau wa elimu

katika ngazi zote za manispaa.

10. Kuandaa Tange ya walimu wa shule za msingi kwa kila mwaka.