Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii

IDARA YA MAENDELEO YA JAMII NA USTAWI WA JAMII

Majukumu ya Idara

1. Kutoa maelekezo na miongozo ya kisera juu ya uanzishaji wa

vikundi vya uzalishaji mali ya wanawake.

2. Kusanifu miradi midogo ya uzalishaji mali ya vikundi vya

wanawake na kutoa ushauri wa kitaalamu.

3. Kutoa ushauri wa kitaalam na kupitisha maombi ya vikundi vya

kiraia na NGOs kufungua A/C Benki.

4. Kupokea na kutatua migogoro ya ndoa ndani ya kulingana nahali

ya mgogoro/kesi ilivyo.

5. Kushughulikia kesi za watoto na kusimamia haki zao za msingi

kisheria, ulinzi na usalama wao.

6. Kushirikiana na wadau mbalimbali kupokea nyaraka za kesi

kulingana na umuhimu wa rufaa hiyo ili kupata msaada zaidi.

7. Kukagua vituo vya kulea watoto (day are centre) na makao ya

watoto (children’s homes)

8. Kushirikiana na vyama vya watu wenye mahitaji maalum ili

kusimamia haki zao za msingi kwa muda muafaka.