Idara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

IDARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI

Majukumu ya Idara ya mifugo na uvuvi

1. Kuwatembelea wafugaji ili kutoa ushauri wa kitaalam katika

maeneo yao ya kazi.

2. Kutoa chanjo ya kichaa cha mbwa na paka.

3. Kukagua nyama katika machinjio ya Bweri,Kigera na Mwisenge

saa 1:00 asubuhi baada ya kuchinja kila siku.

4. Kutoa matibabu ya mifugo na kufanya uchunguzi wa ugonjwa.

5. Ukaguzi wa afya ya mifugo na mazao yake

6. Utambuzi wa magonjwa, ufuatiliaji na utoaji wa kinga

7. Kutoa ushauri na elimu bora juu ya mifugo

8. Kuandaa taarifa za idara za mwezi, robo mwaka na mwaka

9. Kufuatilia na kutekeleza miradi ya maendeleo ngazi ya kata na

Halmashauri

10. Kufanya utambuzi na usajili wa mifugo na kuhuisha takwimu za

mifugo

11. Kusimamia sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na

kanuni zake za mwaka 2009.

12. Kutoa elimu kwa vikundi vya kusimamia na kuendeleza rasilimali

za Ziwa Victoria (BMUS) ili kufahamu faida za uvuvi endelevu na

athari za uvuvi haramu.

13. Kufanya doria nchi kavu na ziwani (Ziwa Victoria) kwa lengo la

kupambana na uvuvi haramu.

14. Kutoa elimu ya kisasa juu ya ufugaji wa samaki.

15. Kutoa leseni za mitumbwi na ukusanyaji wa samaki.

16. Kutoa vibali vya usafirishaji wa mazao ya uvuvi ndani na nje ya

Manispaa ya Musoma.