Idara ya Mipango Miji na Ardhi

IDARA YA MIPANGO MIJI, ARDHI NA MALIASILI

Idara hii inalo jukumu la kuhakikisha rasilimali Ardhi inatumika 

ipasavyo na wananchi wa Manispaa hii kwa kuwapatia maeneo

yenye makazi salama na tulivu. Aidha pia iwe ni mtaji wa

mwananchi kuweza kukopesheka kwenye Taasisi za fedha baada ya

kupatiwa Hati ya kumiliki.

Majukumu hayo ni:-

1. Kutambua Ardhi iliyoiva kwa matumizi kusudiwa

2. Kuandaa mpango Mkuu wa mipango ya kina ili kuelekeza ukuaji

wa mji

3. Kuandaa michoro ya Mipango miji kwa ajili ya matumizi

4. Kupima maeneo kwa ajili ya viwanja

5. Kutambua thamani ya Ardhi

6. Kufanya uthamini kwa madhumuni mbalimbali

7. Kusimamia ulipaji fidia kwa kuzingatia misingi ya haki

8. Kutayarisha Hati za kisheria

9. Kupendekeza vibali vya upangishaji wa milki, uhamisho, uwekaji

rehani

10. Kuratibu masuala ya Ardhi juu ya Elimu kwa Umma

11. Kushughulikia matumizi ya Ardhi

12. Kunakiri na kuchora michoro ya Mipango miji

13. Kuweka kumbukumbu za michoro ya Mipango miji

14. Kukusanya kodi ya Ardhi

15. Kufanya ukaguzi wa viwanja na kutoa notisi ya kupendekeza

ubatilishaji wa milki kwa viwanja visivyoendelezwa

16. Kutatua migogoro ya Ardhi na mapendekezo Serikalini

17. Kusimamia utekelezaji wa sera, kanuni, miongozo na viwango

vya kuboresha mazingira ya mji

18. Kukuza ushirikiano baina ya Taasisi mbalimabli zinazojihusisha

na maendeleo ya mji Kitaifa na kimataifa

19. Kuandaa bajeti ya Idara na kuandaa vikao vya Idara

20. Kuhakiki na kukagua Hoteli za kitalii zinakidhi vigezo na viwango

vinavyohitajika na watali