Kitengo cha Sheria na Usalama

KITENGO CHA SHERIA

Majukumu ya Kitengo cha Sheria

1. Kufuatilia ,Kusimamia na kutetea kesi za Halmashauri ya

Manispaa zilizoko Mahakamani baada ya siku 1 tu kuwepo kwa

kesi hizo Mahakamani na kuzingatia taratibu za uendeshaji wa

kesi Mahakamani .

2. Kuandaa na kusajili nyaraka za kimahakama zinazohusiana na

kesi zilizoko Mahakamani baada ya siku 21 baada ya kupokea

hati za madai .

3. Kusimamia shia mama na sheria ndogo za halmashauri kwa

kuchukua hatua za kisheria kwa wanaokiuka sheria ndani ya

mamlaka ya Halmashauri ikiwa ni pamoja na kuwafikisha polisi

na Mahakamani baada ya kuwapatia notisi ya siku 30 za kutii

sheria zilizopo na kuonekana wanakaidi.

4. Kusimamia Mabaraza ya kata na kutoa semina elekezi mara kwa

mara kwa wajumbe wa Mabaraza ya Kata .

5. Kuandaa rasimu ya sheria Ndogo na au kufanya marekebisho ya

sheria Ndogo zilizopitwa na wakati ndani ya siku 7 baada ya

kupata mapendekezo kutoka kwenye menejimenti.

6. Kutoa elimu au taarifa kwa umma kuhusu sheria Ndogo za

Halmashauri zinazokusudiwa kutungwa siku 14 kabla ya

halmashauri kupitisha sheria hizo.