Kitengo cha Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Uhusiano

KITENGO CHA TEKNOLOJIA HABARI NA MAWASILIANO NA UHUSIANO

Majukumu ya Kitengo cha Habari na Mawasiliano

1. Kitengo cha Habari, na Mawasiliano kina jukumu la kuhakikisha

Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa inadumisha

mahusiano chanya na wadau wake wa ndani na nje.

2. Kutangaza shughuli zote za serikali na kuujulisha umma shughuli

za maendeleo zinazotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa

ya Musoma kwa njia mbalimbali zikiwemo magazeti, majarida,

vitabu, vipeperushi, radio, TV na tovuti.

3. Majukumu mengine ya msingi ya Kitengo yanahusu kusimamia,

kuratibu na ushauri wa matumizi ya teknolojia ya kompyuta.

Kusimika Mfumo wa Kompyuta wa Kuhifadhi taarifa na

Kumbukumbu za Watumishi na Mishahara (Intergrated

Human Capital Management System); pamoja na utekelezaji wa

Sera ya Serikali Mtandao (e-government policy) katika utumishi

wa umma

4. Aidha, Ofisi hii ina jukumu la kupokea na kushughulikia

malalamiko ya wadau yanayohusu Ofisi ya Mkurugenzi wa

Manispaa.