Obtain Building Permit

Kupata Kibali Cha Ujenzi

Ili kupata kibali cha Ujenzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma utaratibu ufuatao sharti ufuatwe na mwombaji wa kibali husika:-

1. Mwombaji anatakiwa kuwasilisha ramani iliyochorwa na Msanifu Majengo aliyesajiliwa (Registered Achtect).

2. Mwombaji anatakiwa kuambatanisha nakala ya hati ya kiwanja/ ofa au barua kutoka kwa Mtendaji wa Kata wa eneo husika kwa maeneo yasiyopimwa (Squarters)

3. Mwombaji anatakiwa kuzalisha nakala nne za ziambatisho tajwa hapo juu.

4. Mwombaji anatakiwa kuwasilisha nakala nne za majalada zilizo na nyaraka zote zinazohitajika kwa mhandisi wa Manispaa.

5. Mwombaji anatakiwa kuambatanisha nakala za risiti za malipo ya kiwanja angalau risiti mbili za karibuni.

Angalizo: Vibali vyote vya ujenzi vinaidhinishwa na kamati ya Mipango Miji na Mazingira baada ya kukamilika kwa taratibu zote za awali. Aidha, baada ya kukamilika kwa kibali mwombaji atataarifiwa kwa njia ya simu kufika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa kuchukua kibali chake.