Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii

Mfuko wa Afya ya Jamii

Halmashauri ya Manispaa ya Musoma ni miongoni mwa Halmashauri nchini zinazotekeleza mpango wa uchangiaji wa gharama za afya ujulikanao kama mfuko wa Afya ya jamii.

Mfuko wa Afya ya Jamii CHF/TIKA ni mpango wa uchangiaji huduma za matibabu kwa kaya kabla ya kuugua.

Mpango huu unalenga katika kufanikisha azma ya serikali kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za afya na wanazozimudu na kwa usawa

Lengo la Mpango

Mpango huu ulibuniwa  kwa lengo la kuwaepusha wananchi walio wengi na utaratibu wa kuchangia fedha kwa utaratibu wa papo kwa papo kila mara wanapougua au kuuguliwa katika kipindi ambacho hawana fedha.

Walengwa wa Mpango na nani?

Mpango unalenga wananchi wote ambao hawasajiliwa na mifuko mingine ya Afya na ambao hawapo katika sekta rasmi.

Manufaa ya kujiunga na CHF/TIKA

Miongoni mwa manufaa yanayopatikana kwa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii ni yafuatayo:-

  • Watu sita katika kaya watapata matibabu katika vituo vya afya na zahanati za jirani kwa mwaka mzima kwa gharama Tsh. 10,000 pekee.
  • Familia inapata uhakika wa kupata matibabu muda wote ndani ya mwaka mzima hata wakati fedha haipo
  • Kaya inaepuka na malipo ya papo kila mwanakaya anapougua.
  • Kaya iliyo na wanakaya zaidi zaidi ya sita wanafursa ya kulipia waliozidi katika idadi hiyo.

Makundi mengine yaliyo na fursa ya kujiunga na CHF/TIKA

Wanavyuo na wanafunzi walio masomoni na hawajasajiliwa katika mifuko mingine ya bima ya afya.

Wapi utajiunga/Kujiandikisha?

Kila mkuu wa kaya afike katika kituo cha afya au zahanati iliyo jirani asajiri na kupewa kadi itakayowezesha kaya yake kutibiwa kila wanapougua.