NMB Bank donates Medical Equipment worth 5 Mil.

Posted on: March 24th, 2017

Benki ya NMB Yasidia Vifaa Tiba vyenye Thamani ya Mil. 5

Benki ya NMB imeikabidhi Halmashauri ya Halmashauri ya Manispaa ya Musoma vifaa tiba vyenye thamani ya  Shilingi Milioni 5 katika hafla iliyofanyika katika kituo cha afya Nyasho

Vifaa hivi vimetolewa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya mchango wake wa maendeleo kwa jamii. Makabishiano hayo yaliongozwa  na Mgeni rasmi Mheshimiwa Dr. Vicent A. Naano  ambaye ni mkuu wa wilaya ya Musoma.

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameupongeza uongozi wa benki hiyo kwa jitihada zao za kuharakisha maendeleo kwa misaada wanayoitoa katika nyakati tofauti. 

Aidha, Dr. Naano ameualifu uongozi wa benki hiyo kuwa serikali ina mpango wa kufanya upanuzi wa kituo hicho kwa kujenga jengo kubwa na la kisasa kwa lengo la kupanua na kuboresha huduma zitolewazo kituoni hapo.

Dr. Naano amewataka watumishi wa kituo cha afya cha Nyasho kuvitumia vifaa hivyo kwa umakini ili kuviwezesha kudumu kwa muda mrefu.

Vifaa vilivyotolewa ni Vitanda sita vyenye magodoro yake, Vitanda maalum vya kujifungulia akina mama viwili na Viti vyenye magurudumu (Wheel chairs) viwili.