Tunafanya Nini

MAJUKUMU YETU HALMASHAURI YA MANISPAA

 1. Kusimamia na kudumisha amani, ulinzi na usalama katika maeneo ya mipaka yake.
 2. Kuhamasisha/kuendeleza na kuwapatia huduma bora za kijamii na kiuchumi wananchi walio katika eneo la mipaka ya Halmashauri.
 3. Kusimamia utekelezaji wa sera za maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yao.
 4. Kuchukua hatua madhubuti za kuendeleza na kuhifadhi mazingira.
 5. Kusimamia Utawala,fedha mambo yote ya uendeshaji katika ngazi mbalimbali zilizo ndani ya mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa.
 6. Kusimamia na kuhakikisha demokrasia inadumishwa katika jamii.
 7. Kukusanya mapato yatakayowezesha mamlaka ya serikali ya mtaa kuendesha shuguli zake pamoja na kutoa taarifa za matumizi kupitia kamati mbalimbali.
 8. Kutoa huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kutekeleza shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
 9. Kuzingatia na kutambua masuala mtambuka kama vile jinsia.
 10. Kuendeleza na kusimamia kanuni za biashara, viwanda na kilimo.
 11. Kubuni mikakati ya kupambana na umaskini pamoja pamoja na mbinu za kusaidia kuboresha maisha ya vijana, wazee na walemavu
 12. Kusimamia na kuendeleza huduma za afya, elimu, maji, utamaduni na masuala ya burudani katika jamii.