• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Mrejesho |
    • Lalamika |
Musoma Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Wasifu wa Kijamii na Kiuchumi wa Halmashauri
      • Viongozi wetu
        • Mayors
        • Municipal Directors
    • Dira na Dhamira
    • Maadili yetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Usimamizi na Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Uhifadhi Maliasili na Mazingira
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
          • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
            • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Maeneo ya Viwanda
    • Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za maji
    • Maombi ya Huduma
    • Uthibi wa Mazingira
    • Uthibiti wa Misitu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili ya Madiwani
    • Ratiba ya vikao
  • Miradi
    • Miradi inayopendekezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mwongozo wa kushughulikia Malalamiko
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
    • Wasifu wa Kijamii na Kiuchumi wa Halmashauri
    • Miongozo na Nyaraka
    • Sheria ndogo
    • Majarida
    • Council Budget
      • New menu item
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba
    • Makala

Naridhika na Utendaji wenu - Meya

Imewekwa: February 15th, 2021

Naridhika na Utendaji Wenu – Meya

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma Mhe. William Patrick Gumbo amewapongeza watumishi wa Halmashauri kwa kazi nzuri wanayoifanya kuwahudumia wananchi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mhe. Gumbo ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa baraza la wafanyakazi lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.

Akilihutubia baraza hilo, Mhe. Gumbo aliwaasa wawakilishi wa watumishi wanaounda baraza hilo kuwa wakati umefika baraza la wafanya kazi litumike kuongeza tija na kupanga malengo ya maendeleo ya Halmashauri.

“Mara nyingi sisi wanasiasa tunapenda kuona matokeo,” Alisema Mhe. Gumbo.

Aidha, Mhe. Gumbo aliwakumbusha watumishi mafanikio ya Halmashauri kwa miaka mitano iliyopita ambapo Halmashauri ilipata tuzo mbalimbali kwa utendaji uliotukuka kutoka baraza la famasia na maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika kitaifa Mkoani Simiyu.

“Suala la ubunifu katika utendaji wenu ni muhimu, fanyeni mambo ya ziada yatakayoacha alama,” Alisisitiza Mhe. Gumbo.

Aliwataka watumishi kuongeza maarifa katika kuzikabili changamoto na kuongeza kuwa “Ni matumaini yangu kuwa mwisho wa baraza hili mtakuja na michango mizuri pamoja na mapendekezo thabiti”.

Mhe. Gumbo pia alitoa tahadhali kwa wajumbe wa baraza la wafanyakazi kwa kuwataka kuitisha vikao katika idara na vitengo vyao, uharaka wa utoaji huduma kwa wakati pamoja na kuzingatia huduma kwa wateja.

“Tuwe na lugha nzuri kwa wateja pamoja na weledi,” Aliongeza Mhe. Gumbo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi kuzindua baraza la wafanyakazi, mwenyekiti wa baraza Bi. Fidelica Myovella ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa alisema kuwa baraza linalozinduliwa litahudumu kwa muda wa miaka mitatu.

Bi. Myovella alisema baraza la wafanyakazi lina jukumu kubwa kuhakikisha masuala muhimu ya wafanyakazi yanapewa msukumo kutokana na uwakilishi wa watumishi katika kila idara na sekta katika Halmashauri ya Manispaa.

Bi. Myovella alidokeza kuwa kazi kubwa baada ya uzinduzi wa baraza itakuwa kujadili na kupitisha mpango na bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Kabla ya uzinduzi wa baraza kulifanyika uchaguzi wa viongozi wapya wa baraza kwa mujibu wa mkataba wa baraza ambapo Bi. Aines Anderson alichaguliwa kuwa katibu mpya wa baraza huku Ndugu Benedict Balole akichaguliwa kuwa katibu msaidizi.

Baraza la wafanyakazi linauhishwa baada ya baraza lililokuwepo kukamilisha muda wake.  

Matangazo

  • Terms of Reference for the provision of construction supervision consultancy services for urban infrastructure development in Musoma Municipality under the TACTIC Project March 06, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA MTENDAJI WA MTAA III October 05, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI WA MAHOJIANO October 03, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI WA MAHOJIANO October 03, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mvua iliyoambatana na upepo yasababisha maafa Manispaa ya Musoma

    March 24, 2025
  • UKAGUZI WA MIRADI

    November 05, 2024
  • Watumishi waaswa kuchapa kazi bila kujali uchache wao

    September 08, 2022
  • Dc musoma ataka ubunifu katika uanzishaji wa miradi ya kuongeza kipato

    September 08, 2022
  • Tazama zote

Video

Hotuba ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara
Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sisi ni nani
  • Dira na Dhamira

Viunganishi Linganifu

  • IKULU
  • Tovuti ya Mikopo ya wajasiriamali
  • Public Service Management
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Musoma Municipal Council

    Sanduku la Posta: Box 194 Musoma

    Simu: 0282622560

    Simu ya Mkononi: +255754013734

    Barua pepe: info@musomamc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.