• Wasiliana Nasi |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • feedback |
    • Complain |
Musoma Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Musoma Municipal Council

  • Home
  • About Us
    • History
      • Social Economic Profile
      • Our Leaders
        • Mayors
        • Municipal Directors
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Departments
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Department of Community Development and social Welfare
      • Idara ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
    • Units
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Internal Audit Unit
      • Kitengo cha Usimamizi na Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Uhifadhi Maliasili na Mazingira
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
          • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
            • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industrial Areas
    • Transportation
  • Our services
    • Health
    • Education
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fisheries
    • Water facililies
    • Application for services
    • Environmental management
    • Forest Management
  • Councilors
    • List of Councillors
    • Standing Committees
      • Finance and Administration Committee
      • Education, Health and Economic Services Committee
      • Town Planning and Environment Committee
      • HIV AIDS Control Committee
      • Councillors Integrity Committee
    • Meeting schedule
  • Projects
    • Proposed Projects
    • On Going Projects
    • Completed Projects
  • Publications
    • Reports
    • General Planning Scheme
    • Client Service Charter
    • Council Grievances Guidelines
    • Forms
    • Strategic Plan
    • Social Economic Profile
    • Securals and guidelines
    • By Laws
    • Journals
    • Council Budget
      • New menu item
  • Media Center
    • Video Gallery
    • Photo Gallery
    • Releases and Statements
    • Speeches
    • Feature Articles

RC Envisions New Musoma

Posted on: June 14th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Kigoma Malima amelitaka baraza la Madiwani kutekeleza wajibu wake wa kuisimamia Halmashauri kwa kuweka mbele agenda ya maendeleo ili kufukia malengo.

Mhe. Malima ameyasema hayo alipokuwa akilihutubia baraza la Madiwani katika mkutano maalum wa kujadili hoja za ukaguzi uliofanyika jana katika ukumbi mkuu wa Manispaa ya Musoma.

Mhe. Malima amesisitiza kuwa Manispaa ya Musoma lazima ibadilike and kuongeza kuwa ili kufikia maendeleo lazima viongozi na wataalam wajiulize maswali magumu yatakayopelekea kupata suluhisho la changamoto zinazokabili ukuaji wa Manispaa.

Aidha, alitahadhalisha kuwa bila kubadilika Musoma itakuwa Mji wa mwisho miaka michache ijayo.

“Maendeleo yana kazi kubwa, hapa ni ‘capital city’, ninyi ni wajanja tuzungumze basi mambo ya maendeleo”. Alisema Mhe Malima.

Pamoja na kuibadili Musoma kwa mtizamo wa maendeleo aliwataka madiwani wasimame kwenye kilele cha ukweli na haki ili kusimamia kwa ufanisi shughuli zote za maendeleo katika Manispaa.

Kuhusu Uwajibikaji wa Mashirika ya Umma

Mhe. Malima aliweka wazi dhamira yake ya kuyasimamia mashirika na taasisi zote zilizo chini yake na kuzitaka kuzingatia misingi ya uwajibikaji na weledi.

Mhe. Malima aliitolea mfano Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira(MUWASA) ambayo haikuwa na utendaji wa kuridhisha hatua iliyopelekea kuvunjwa kwa bodi yake na kusimamishwa kwa baadhi ya watendaji.

“Simuombi mtu radhi kwa MUWASA kwa sababu ndilo shirika langu nyeti, nikiona uozo lazima niseme, kuna watu nimewashika kubaya” alisema na kuongeza “ Na mimi nawajua wapigaji, nimewashika pabaya, siombi msamaha kwa jambo lililo kwenda vibaya”. Alisema Mhe. Malima.

“Kuna wabaya wanapeleka maneno kuwa yule jamaa anaondoka muda wowote, waambieni wanapoteza muda. Kila mtu abebe mzigo wake”.Alisisitiza Mhe. Malima.

Mhe. Malima alimtaka  kila anayehusika kuhakikisha anasimamia eneo lake na kuondoa dosari zote za kiutendaji zinazoweza kuleta maswali yasiyo na majibu kwa wananchi.

Uvuvi Haramu

Kuhusu uvuvi haramu Mhe. Malima alisema kuwa adui mkubwa  wa viwanda vya samaki ni uvuvi haramu na kuwataka wote wanaohusika kuacha mara moja vitendo hivyo.

Mhe. Malima aliongeza kuwa kiwanda cha ‘Prime Catch’ kilikuwa kinatoa ajira 700 lakini kutokana na uvuvi haramu samaki walipungua na hivyo uzalishaji wa kiwanda ulishuka hali  iliyopelekea kufungwa kwa kiwanda hicho na ajira kupotea.

“Ukimjua ndugu yako anafanya uvuvi haramu mwambie Mkuu wa Mkoa atabanana nae kila kona”. Alionya Mhe. Malima.

Upanuzi wa Uwanja wa ndege, eneo la Utawala na uwekezaji

Akizungumza kuhusu uwanja wa ndege Mhe. Malima lazima Manispaa ya Musoma iwe na uwanja wa ndege kwa maslahi mapana ya kiuchumi na  kuzihudumia kwa ufanisi rasilimali za hifadhi ya taifa ya Serengeti.

Aliendelea kufafanua kuwa Musoma bila uwanja wa ndege haiwezi kupiga hatua kwa kuwa Musoma ndio pointi ya karibu kufika hifadhi ya Serengeti hivyo uwepo wa uwanja wa ndege utawavutia watalii wengi na fursa nyingine nyingi.

“Tunapozungumza kuhusu musoma lazima tujue tunalo tatizo kubwa.Musoma inazo rasilimali za pekee”. Alisema Mhe. Malima.

Mbali na rasilimali nyingi zilizoko Musoma wawekezaji wengi wamekuwa wakielekea mikoa ya jirani na mara nyingine kuhamisha biashara zao Musoma.

“Nataka wote tujiulize kwa nini watu hawawekezi Musoma?” aliuliza Mhe. Malima na kuongeza kuwa “Lipo tatizo na nawaambieni maneno magumu, makali, ili mjitafakari wenyewe, nyie ndio mliopewa dhamana na wananchi”.

Mhe. Malima alihitimisha hotuba yake kwa kulitaka baraza la Madiwani kuchukua hatua za makusudi kupanua eneo la Utawala la Manispaa kwa kufuata taratibu zote ili kuisaidia musoma kukua na kupata eneo la kupumulia.

“Lazima tukae kama madiwani tuchukue dhamana ya maendeleo ya mji wa Musoma. Nendeni mkaongee na jeshi na Halmashauri za jirani mpate maeneo ya viwanda na uwekezaji”. Alisema Mhe. Malima.

Awali akifunga mkutano wa Baraza la Madiwani Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma Mhe. William Gumbo alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa  maelekezo na ushauri wake kwa maendeleo ya Manispaa ya Musoma na kuahidi kuchukua hatua kuanzia sasa ili kuibadilisha Musoma.  

Announcements

  • Terms of Reference for the provision of construction supervision consultancy services for urban infrastracture development in Musoma Municipality under the TACTIC Project March 06, 2025
  • WRITTEN INTERVIEW RESULTS FOR MTENDAJI WA MTAA III October 05, 2024
  • CALL FOR ORAL INTERVIEW October 03, 2024
  • CALL FOR ORAL INERVIEW October 03, 2024
  • View All

Latest News

  • Hurricane affects property in Musoma Municipal Council

    March 24, 2025
  • PROJECT SUPERVISION

    November 05, 2024
  • Watumishi waaswa kuchapa kazi bila kujali uchache wao

    September 08, 2022
  • Dc musoma ataka ubunifu katika uanzishaji wa miradi ya kuongeza kipato

    September 08, 2022
  • View All

Video

Hotuba ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara
More Videos

Quick Links

  • Who we are
  • Vision and Mission

Related Links

  • State House
  • Tovuti ya mikopo ya wajasiriamali
  • Public Service Management
  • PO-RALG
  • National Bereau of Statistics
  • Tanzania Information Services

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Musoma Municipal Council

    Postal Address: Box 194 Musoma

    Telephone: 0282622560

    Mobile: +255754013734

    Email: info@musomamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.